Sunday, December 23, 2012

WAZAYUNI WABANA VYOMBO VYA HABARI VYA IRAN

Kwa mara nyingine nchi za Magharibi zinazodai kuwa na uhuru wa kusema zimefungia vyombo vya habari vya Iran ili sauti huru isiwafikie walimwengu. Weledi wa mambo wanaamni kuwa, lobi za utawala wa Kizayuni wa Israel katika nchi za Magharibi ndizo zinazopelekea kubanwa vyombo hivyo vya habari vya Iran. William Spring, mwanaharakati wa haki za binaadamu ameiambia televisheni ya Press TV kuwa lobi za Wazayuni nchini Marekani ndizo zinazoshinikiza kubanwa vyombo vya habari vya Iran. Mara kwa mara nchi za Ulaya zimekuwa zikifungia kurushwa hewani vyombo vya habari vya Iran ikiwemo Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran, televisheni za Press TV, al Alam, Hispan TV n.k, kwa madai yasiyo na msingi dhidi ya Shirika la Sauti na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB. Kwa upande wa Idhaa ya Kiswahili radio Tehran, imeshatolewa mara kadhaa kwenye satalaiti kama vile Hortbird, Intelsat n.k bila ya taarifa yoyote. William Spring pia amesema kuwa, hivi sasa utawala wa Kizayuni unahisi unazidi kushindwa na vyombo vya habari vinavyotangaza ukweli kuhusu jinai za Israel na siasa za kibeberu duniani na kwamba hii inaonesha ni kiasi gani Wazayuni wana ushawishi katika siasa za mambo ya nje za Marekani.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO