Thursday, December 20, 2012

BIDEN KUONGOZA JOPO LA UCHUNGUZI WA MAUAJI YA NEWTON

Rais  Barack Obama  leo atamteua makamu  wa  Rais Joe Biden  kuongoza  jopo  ambalo  litakuwa  na  wajibu  wa kutayarisha  sera  mpya  zitakazoshughulikia  masuala  ya ghasia zinazosababishwa  na  matumizi  ya  silaha  baada ya  mauaji  katika  shule  moja  nchini  Marekani  wiki iliyopita. Afisa  wa  Ikulu  ya  Marekani  ameliambia  shirika la  habari  la  AFP  kuwa  Obama  atamteua  rasmi Biden kuongoza  jopo  litakalojumuisha  mashirika  mbali  mbali baadaye  leo katika hafla itakayofanyika kwenye Ikulu hiyo. Rais Obama hatarajiwi  kutaja  uamuzi  wowote  wa sheria mpya  wakati wa  hafla hiyo. Badala  yake, jopo  hilo litajaribu  kupanga  sera  mpya  baada  ya  mashambulizi ya silaha  katika  shule  mjini  Newtown, Connectcut, ambapo  kijana  mwenye  umri  wa  miaka  20 alimpiga risasi mama  yake, pamoja  na  watoto  20  pamoja  na watu  wazima  sita  katika  shule  ya  msingi  ya  Sandy Hook.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO