Thursday, December 20, 2012

MULIKUWA WAPI WAKATI IRAN IKISTAWI KISAYANSI


Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema harakati ya sayansi Iran ilinawiri na kustawi wakati nchi za Magharibi zilipokuwa katika kiza.
Katika ujumbe wake kwa Kongamano la Kimataifa la Qutb al-Din al Shirazi, Kiongozi Muadhamu amesema kuna udharura wa kutoa ufafanuzi kuhusu zama za ustawi wa kisayansi na kimaarifa na kuarifisha shakhsia wakubwa wa kisayansi ili wawe vigezo kwa kizazi cha leo.
Qutb al-Din al-Shirazi alikuwa mwanasayansi wa Kiislamu aliyeishi Iran katika karne ya nane Hijria Qamaria sawia na karne za 13 na 14 Miladia. Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema katika kipindi hicho nuru ya sayansi ilikuwa bado haijaangazia bara Ulaya. Kongamano la Kimataifa la Qutb al-Din al Shirazi linafanyika katika mji wa Shiraz kusini mwa Iran kwa mnasaba wa mwaka wa 800 wa kuadhimisha siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa mwanazuoni na malenga huyo wa Uajemi. Kongamano hilo la siku mbili lililoanza Jumatano linahudhuriwa na wasomi kutoka nchi tisa.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO