Wednesday, December 19, 2012

VIONGOZI WA UAMSHO DHAMANA BADO YAKATALIWA


Kesi inayowakabili viongozi wakuu wa jumuiya ya Uamsho iliyoendeshwa leo katika mahakama kuu ya vuga mjini zanzibar imelikataa ombi la dhamana na kupelekea viongozi hao kurudi tena rumande. Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo mnamo majira saa mbili na nusu asubuhi huku wakiwa chini ya ulinzi mkali uliokua ukiongozwa na gari tatu za FFU pamoja na baadhi ya askari wa vikosi vya kmkm. Katika kesi hiyo jaji Mkusa Sepetu amelazimika kulikataa ombi la dhamana kwa washtakiwa hao ambalo lilikua likifuatiliwa kwa muda mrefu lakini lilikuwa likiwekewa pingamizi tofauti.

Amebainisha kuwa ombi hilo limekataliwa kwa madai kuwa halikufuata taratibu sahihi za kisheria, Hivyo mahakama imewataka watetezi wa wateja hao kufuata taratibu zilizo sahihi juu ya ombi lao la kupatiwa dhamana viongozi hao. Kwa upande wa uteteze wawashtakiwa hao kimsingi haukufurahishwa na maamuzi yalioamuliwa na mahakama hio yakulitupilia mbali ombi hilo la dhamana kwani wamesema hoja iliotolewa uamuzi si miongoni mwa hoja iliowasilishwa kwa dpp kimsingi wamesema ni hoja ilioibuliwa na mahakama wenyewe jambo ambalo linawapa mashaka mawakili hao.
Aidha wamesema kuwa wallipanga kuwasilisha ombi jipya leo hii la kudai dhamana kwa wateja wao lakini kutokana na muda kutokuruhusu kwa siku ya leo Wameamuwa kujipanga upya zaid na kuwasilisha maombi hayo hapo kesho.
Kesi hiyo itasikilizwa tena mnamo tarehe 3/1/2013

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO