Balozi wa Iran nchini Russia ameelezea uwezekano wa Iran kuwaruhusu wakaguzi wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia IAEA kutembela kituo cha kijeshi cha Parchin kwa masharti. Muhammadreza Sajjadi ameeleza kuwa, baada ya Iran kusaini protokali maalumu na wakala wa IAEA itawapa ruhusa wakaguzi wa taasisi hiyo kutembela kituo cha kijeshi cha Parchin.
Parchin si miongoni mwa vituo vya nyuklia vya Iran na kwa mujibu wa sheria za wakala wa IAEA Tehran hailazimiki kuruhusu maafisa wa wakala huo kukagua kituo hicho cha kijeshi. Hata hivyo, wakaguzi wa wakala huo mwaka 2005 walitembelea kituo hicho kilichoko mashariki mwa mji mkuu Tehran mara mbili na matokeo ya ukaguzi wao yalionesha kuwa hakuna shughuli zozote za nyuklia zinazofanyika kwenye kituo hicho. Balozi wa Iran nchini Russia amesisitiza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu kamwe haitosimamisha urutubushaji urani na pia kwamba haitofunga kituo chake cha nyuklia cha Fordo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO