Thursday, December 13, 2012
BOKO HARAMU WEKA SILAHA CHINI
Jeshi la Nigeria limewataka wanachama wa kundi la Boko Haram kuweka chini silaha na kufuata mwenendo wa amani kwa lengo la kurejesha hali ya usalama nchini humo. Mkuu wa Majeshi nchini Nigeria Admiral Ola Sa'ad Ibrahim aliyewasili mjini Maiduguri kwa ajili ya kuangalia uharibifu uliofanywa na kundi la Boko Haram katika eneo la Brono huko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, amenukuliwa akisema kuwa, ikiwa kundi hilo lina uwezo mkubwa kama linavyodai, basi lazima liachane na vitendo vya ukatili na badala yake liwe kundi la kisiasa. Ibrahim amesema kuwa, mji wa Brono umezorota kutokana na mashambulizi ya kundi hilo la Boko Haram na kwamba, shughuli zote zinazofanywa na kundi hilo zinapingana kabisa na misingi ya sheria za Kiislamu. Hivi karibuni Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan alitangaza kuwa, serikali yake imejiandaa kufanya mazungumzo na Boko Haram kwa ajili ya kurejesha hali ya utulivu nchini.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO