Monday, December 17, 2012

HISTORIA YA KRISMASS NA HUKUMU YA KUSHEREHEKEA


Wakati wa zama za kale, siku ya mwisho ya majira ya baridi huko sehemu za Kusini kulisherehekewa mfano wa usiku ambao mungu wa Mama Watakatifu alijifungua mtoto akijulikana kuwa ni mungu wa Jua. Pia (siku hii) inaitwa Yule, siku ambayo inasherehekewa mno kwa kurushwa pashpashi. Ambapo kila mtu atacheza na kuimba ili kuliamsha jua kutokana na usingizi wake mnono wa majira ya baridi. Wakati wa Warumi, iliadhimishwa kwa kumsifu Satunusi (mungu wa mavuno) na Mithrasi (mungu wa kale wa nuru), huo ni mtindo wa kuabudia jua ambao umekuja ukitokea Syria hadi Urumi. Karne kabla ya madhehebu ya Sol Invictus, ilitangaza ya kwamba, majira hayo ya baridi sio ya milele, na kwamba maisha yanasonga mbele, na ni mualiko wa kubaki kwenye nguvu nzuri. Siku ya mwisho ya majira ya baridi huko sehemu za mviringo za Kusini ni baina ya siku ya 20 au 22 Disemba. Warumi waliadhimisha Saturnalia baina ya tarehe 17 na 24 Disemba.
http://www.alhidaaya.com/sw/node/6043

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO