Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel kwa mara nyingine tena limekiuka makubaliano ya kusimamisha vita kati yake na Wapalestina baada ya kuifyatulia risasi boti ya uvuvi ya Palestina huko kaskazini mwa Ukanda wa Ghaza.
Wanajeshi wa Israel lmapema leo wameifyatulia risasi boti ya uvuvi ya Wapalestina na kumjeruhi abiria mmoja aliyekuweko ndani ya boti hiyo. Wanajeshi wa utawala haramu wa Israel waliifyatulia risasi boti hiyo kwa kisingingizio kwamba ilivuka mipaka iliyoainishwa kwa wavuvi wa Kipalestina.
Wizara ya Kilimo ya serikali halali ya Palestina inayoongozwa na Waziri Mkuu Ismail Hania pia imethibitisha kujeruhiwa mvuvi huyo wa Kipalestina kwa jina la Masoud Abdulrazaq na kutangaza kuwa wanajeshi wa Israel wamemtia mbaroni mvuvi mwingine wa Kipalestina aliyetambuliwa kwa jina la Ad'ham Bakr.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO