Monday, December 17, 2012
IRAN IKO TAYARI KULINDA BAHARI YA KIMATAIFA
Kamanda wa vikosi vya majini vya jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa vikosi hivyo viko tayari kuweko katika maji huru na ya kimataifa yakiwemo maji ya bahari ya Pacific. Admeri Habibullah Sayari ameashiria uwezo wa hali ya juu wa vikosi vya majini vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika uga wa zana za kijeshi na uzoefu na kueleza kuwa vikosi vya majini vya Iran viko tayari kuweko katika maji huru na ya kimataifa ili kudhamini maslahi na usalama wa meli za kibiashara na zile za mafuta. Kamanda wa vikosi vya majini vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa kuweko Iran katika bahari ya Pacific kunajiri kwa mujibu wa sheria za kimataifa na kwa kuzingatia maslahi na taratibu za kawaida na kuongeza kuwa vikosi hivyo viko tayari kuweko katika maji huru na ya kimataifa kwa lengo la kufikisha ujumbe wa amani na urafiki kwa nchi jirani za eneo na nyingine za dunia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO