Monday, December 17, 2012
LIBYA YAFUNGA MIPAKA YAKE
Libya imetangaza kufunga mipaka yake na nchi nne inazopakana nazo. Taarifa iliyotolewa na Kongresi ya Kitaifa ya Libya imebainisha kwamba, Tripoli imechukua uamuzi huo wa kufunga mipaka yake na majirani zake kwa muda kutokana na kuongezeka tafrani ya ukosefu wa amani katika mipaka hiyo. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Libya imefunga mipaka yake na Chad, Niger, Sudan na Algeria. Habari zaidi kutoka Libya zinasema kuwa, Kongersi ya Kitaifa ya Libya itaweka sheria mpya za kuingia na kutoka wasafiri sambamba na uingizaji na utoaji bidhaa katika maeneo hayo ya mpakani. Maeneo ya milimani ya magharibi mwa Tunisia ambayo yanapakana na Algeria, hivi karibuni yalishuhudia mapigano ya silaha baina ya vikosi vya usalama vikishirikiana na jeshi dhidi ya makundi ya wabeba silaha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO