IRAN YAIKAMATA NDEGE YA MAREKANI ISIYOKUWA NA RUBANI
Iran imeikamata ndege ya Marekani isiyokuwa na rubani ambayo ilikuwa ikiruka katika eneo la anga la nchi hiyo. Ndege hiyo ilikuwa ikikusanya taarifa katika eneo la Bahari ya Ghuba na kuingia katika anga ya Iran wakati ilipokamatwa na kikosi cha jeshi la majini.
Jeshi la walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa
nchini limefanikiwa kukamata ndege ya kijasusi ya Marekani isiyo na rubani punde
baada ya kuingia kinyemela katika anga ya Iran.
'Drone' hiyo ijulikanayo
kama Scan-Eagle inasemekana kuwa na teknolojia ya kisasa zaidi ya kueza kuepuka
rada lakini jeshi la Iran limeweza kugundua janjajanja za Washington na
kuikamata ndege hiyo isiyo na rubani.
Wataalamu wa masuala ya kijeshi
wamesema kuwa, Iran imeonyesha ustadi mkubwa kwa kuinasa ndege hiyo ya kijasusi
na kwamba hiyo ni kengele ya hatari kwa Marekani kwamba uwezo wa kijeshi wa Iran
ni mkubwa kushinda wanavyodhania.
Huko nyuma pia jeshi lilifanikiwa
kuangusha ndege nyingine ya Marekani isiyo na rubani baada ya kuingia katika
anga ya Iran bila idhini.
Huku hayo yakijiri, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya
Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Ramin Mehmanparast amekosoa njama mpya ya
kuiwekea Iran vikwazo vipya akisema si mashinikizo wala vikwazo vitaipigisha
magoti serikali ya Iran na kwamba mashindikizo na vikwazo hivyo ni kinyume cha
sheria.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO