Monday, December 10, 2012

ISRAEL ILITAKA KUMUUA KIONGOZI WA jiHADUL ISLAM



Msemaji wa Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina 
amesema kuwa, utawala wa Israel ulipanga njama za kumuuwa Dakta Ramadhan Abdullah Kiongozi wa Jihadul Islami kama angelifuatana na Khalid Mash'al Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Palestina Hamas huko Ukanda wa Gaza. Daud Shahab ameongeza kuwa, utawala wa Israel ulitamka wazi kwamba kama  Dakta Ramadhan Abdullah na ujumbe wake ataelekea huko Gaza, majeshi ya Israel yatatekeleza operesheni ya kumuuwa yeye na ujumbe wake. Utawala wa Israel uliwaarifu viongozi wa Misri kwamba, makubaliano ya usitishaji vita yangelivunjika iwapo kiongozi huyo wa Jihadul Islami angelifanya safari huko Ukanda wa Gaza. Msemaji wa Jihadul Islami ameongeza kuwa, mapambano dhidi ya maghasibu wa Israel yatachukua muda mrefu na kwamba nchi za Kiislamu na Kiarabu zinapaswa kuwaunga mkono wananchi wa Palestina katika mapambano yao dhidi ya Wazayuni. Amesema kuwa, wapiganaji wa Kipalestina hivi sasa wana ari na moyo wa kishujaa wa kukabiliana na utawala wa Israel na kuzitaka nchi za Kiarabu na Kiislamu kuwapatia silaha wanamapambano wa Palestina.

2 comments:

  1. Do you thoughts plainly repost this onto my personal web site?
    I've to make sure credit rating emerged where it's credited.
    Have a good 1!
    My web page ; check Background

    ReplyDelete
  2. Seriously! Appreciate it! It's my job to wanted to produce in my website something of that nature. Am i allowed to have a fragment of one's publish in order to my site?
    Feel free to visit my weblog ... Online Vehicle Insurance

    ReplyDelete

TUPE MAWAZO YAKO