Monday, December 10, 2012

ISRAEL YASHIRIKIANA NA WAASI WA SYRIA

Maafisa wa kijeshi 40 wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameingia nchini Syria kwa shabaha ya kuyasaidia makundi ya kigaidi nchini humo. Marekani imeamua kutuma nchini Syria maafisa hao waliopata mafunzo maalumu ya kupigana kwenye vita vya mitaani, baada ya kuona kwamba makundi hayo ya waasi yanayojulikana kwa jina la 'Jeshi la Ukombozi wa Syria' kushindwa kuuangusha utawala uliochaguliwa na wananchi wa Syria. Taarifa za kijasusi zinaeleza kuwa, maafisa hao 40 mara baada ya kuingia nchini Syria, waligawanyika katika makundi mawili na  wanajeshi 20 walipelekwa katika mkoa wa Halab, kaskazini mwa Syria na wengine waliosalia walipelekwa Damascus, mji mkuu wa nchi hiyo amma kundi lililoelekea Damascus lililazimika kuukimbia mji huo baada ya kushadidi mapigano ya hivi karibuni pambizoni mwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Damascus. Taarifa zimeeleza kuwa, wanajeshi hao wa Israel walilazimika kukimbilia katika mji wa Halab baada ya majeshi ya serikali ya Syria kutekeleza operesheni kubwa ya kuwaangamiza waasi wa nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO