Jeshi la Nigeria limetangaza kuwa, limewatia nguvuni watu 28 wanaodhaniwa kuwa wanachama wa kundi la Boko Haram ambalo limekuwa likifanya mauaji kaskazini mwa ncji hiyo. Taarifa ya jeshi la Nigeria imebainisha kwamba, wanachama hao wa Boko Haram wametiwa mbaroni baada ya ngome yao kushambuliwa katika mji wa Kano. Taarifa zaidi zinasema kuwa, lengo la operesheni za jeshi la Nigeria ni kushadidisha mashinikizo dhidi ya kundi la Boko Haram na kulitokomeza kabisa kundi hilo ambalo limekuwa likihatarisha usalama wa nchi.
Kundi la Boko Haram linatuhumiwa kuhusika na mauaji mengi yaliyofanyika nchini Nigeria, na wanachama wake wamekuwa wakisakwa kwa udi na uvumba na jeshi la nchi hiyo. Hadi sasa mamia ya watu wameshapoteza maisha yao na majengo kadhaa ya serikali na makanisa kuchomwa moto kutokana na mashambulio yanayofanywa na kundi hilo kaskazini mwa Nigeria.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO