Thursday, December 13, 2012

ISRAEL KUNUNUA MAKOMBORA YA GPS TOKA MAREKANI

Serikali ya Marekani bado inachunguza uwezekano wa kuuzia utawala wa Kizayuni wa Israel makombora 6,900 ya GPS yenye thamani ya dola milioni 647. Wakala unaohusika na usalama na ulinzi katika Wizara ya Ulinzi ya Marekani Pentagon umeeleza kuwa, Washington imeahidi kudhamini usalama wa Israel na kuusaidia utawala huo  katika kuimarisha nguvu zake za kijeshi. Duru za kijeshi za Marekani zinaeleza kuwa, Israel inanunua makombora hayo kwa lengo la kujiimarisha zaidi kutokana na uwezekano wa siku za usoni kujitokeza vita dhidi ya Iran. Duru hizo zimeongeza kuwa, ombi la Israel la kununua makombora hayo lilitolewa wakati kulipoongezeka mivutano katika eneo la Mashariki ya Kati juu ya mipango ya nyuklia ya Iran, huku Washington na Tel Aviv na baadhi ya nchi za Magharibi zikituhumu Tehran kuwa eti inataka kuzalisha silaha za nyuklia. Madai hayo yanatolewa katika hali ambayo, viongozi wa Iran na hata wakuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia IAEA wamethibitisha kwamba miradi ya nyuklia ya Iran inafanyika kwa malengo ya amani, tena chini ya usimamizi wa wakaguzi wa IAEA.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO