Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya wamepanga kuchunguza suala la ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi unaoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni katika maeneo ya Palestina. Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya katika kilao chao cha leo huko Brussels mji mkuu wa Ubelgiji wamepanga kuchunguza hali ya mambo ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na utawala wa Kizayuni khususan uamuzi wa hivi karibuni wa utawala wa Kizayuni wa kutaka kujenga nyumba mpya elfu tatu za walowezi wa Kiyahudi huko Baitul Muqaddas na katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo wanasiasa wa Israel wametabiri kuwa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya katika kikao chao hicho cha leo wataridhika tu na kulaani hatua hiyo ya Israel na wala hawatachukua hatua yoyote ya jadi kuhusiana na hatua hiyo ya Israel ya kutaka kujenga nyumba mpya nyingine elfu 3 za walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO