Wednesday, December 19, 2012
KOREA KUSINI WACHAGUA RAIS
Upigaji kura umemalizika hivi sasa nchini Korea ya kusini katika uchaguzi wa rais. Mgombea wa chama tawala cha kihafidhina Park Guen-hye anapambana na mgombea wa upinzani Moon Jae In kutoka chama cha Democratic United Party. Park ambaye ni mtoto wa dikteta wa zamani nchini humo marehemu Park Chung-hee anapewa nafasi ya ushindi ambayo hata hivyo ni finyu katika uchunguzi wa maoni ambao umechapishwa wiki iliyopita. Iwapo atashinda atakuwa kiongozi wa kwanza mwanamke nchini humo ambako wanaume bado wanashikilia nafasi muhimu za madaraka. Lakini Moon, mwanasheria wa zamani wa haki za binadamu na mtoto wa kiume wa mkimbizi kutoka Korea ya kaskazini anasemekana kujiongezea sana umaarufu katika siku za hivi karibuni. Upigaji kura umekamilika na, matokeo ya awali yatatolewa muda mfupi baadaye. Mshindi wa uchaguzi huo atachukua madaraka mwishoni mwa mwezi wa Februari, akichukua nafasi ya rais wa sasa Lee Myung Bak.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO