Wednesday, December 19, 2012

OIC YASEMA WAISLAM SIO MAGAIDI

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Nchi za Kiislamu OIC amesema kuwa dini ya Kiislamu ni dini ya amani na urafiki. Ikmaluddin Ehsanoghlo Katibu Mkuu wa OIC amekosa vitendo vya kigaidi huko kaskazini mwa Mali na kusisitiza kwamba kufanya mauaji na kuzusha machafuko kwa jina la Uislamu ni jambo lisilokubalika. Katibu Mkuu wa Jumuiya ya OIC ameripoti pia kuainishwa Mjumbe Maalumu huko Mali katika fremu ya jitihada za kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa nchi hiyo na kuongeza kuwa  mjumbe huyo anataraji kukutana na pande mbalimbali na kuchunguza njia za kutatua mgogoro wa huko kaskazini mwa Mali. Ikmaluddin Ehsanoghlo pia amezungumzia kuhusu hali ya mambo ya Misri na akasema kuna ulazima mwa kuimarishwa demokrasia nchini humo.  Katibu Mkuu wa OIC pia amezungumzia juhudi za jumuiya hiyo za kutatua matatizo na kukidhi mahitaji ya Waislamu wa kabila la Rohingya huko Myanmar.  

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO