Thursday, December 20, 2012

LEBANON WAKATAA OMBI LA MAREKANI

Wizara ya Mawasiliano ya Posta na Simu ya Lebanon imelikataa ombi la Marekani la kutaka kujenga kituo cha mawasiliano ndani ya ardhi ya nchi hiyo. Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo imeeleza kuwa hatua hiyo inakinzana na misingi ya kidiplomasia na inakiuka pia mamlaka ya kujitawala ya Lebanon. 
Wakati huo huo Faisal Daud, kiongozi wa harakati ya mapambano ya Kiarabu ya Lebanon amesema, kutokana na kugunduliwa mitandao kadhaa ya kijasusi ya utawala wa Kizayuni wa Israel ndani ya ardhi ya Lebanon kujengwa kituo cha mawasiliano ya posta na simu cha Marekani ndani ya ardhi ya nchi hiyo ni hatua ya kwanza ya kutumikia na kudhamini maslahi ya utawala wa kizayuni katika eneo. Wataalamu wa masuala ya kisiasa na usalama katika eneo wanalitathmini ombi hilo la Marekani kuwa ni sehemu ya mkakati wa kijasusi wa Washington dhidi ya muqawama na nchi za eneo la Mashariki ya Kati hususan Syria, na ni kwa sababu hiyo ombi hilo limekataliwa na serikali ya Beirut. Hata hivyo wataalamu hao wanaamini kwamba Washington itaishinikiza zaidi serikali ya Lebanon mpaka ihakikishe inapata kibali cha kujenga kituo hicho

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO