Thursday, December 20, 2012
KURA YA MAONI MISRI BADO YAPINGWA
Muhammad Mahdi Aakif, kiongozi wa zamani wa harakati ya Ikhwanul Muslimin ya Misri ameukosoa msimamo wa makundi ya kisiasa ya nchi hiyo wa kuyakataa matokeo ya awamu ya kwanza ya kura ya maoni ya katiba na kusisitiza kwamba takwa la wapinzani hao la kutaka kubatilishwa kura hiyo ya maoni halina msingi. Matokeo ya awamu ya kwanza ya kura ya maoni ya katiba mpya ya Misri yanaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 56 ya wapiga kura wameunga mkono rasimu ya katiba hiyo kulinganisha na asilimia 43 walioipinga. Kiongozi wa zamani wa Ikhwanul Muslimin amesema msimamo wa mirengo ya kisiasa wa kung’ang’ania takwa lao la kubatilishwa kura ya maoni na kuundwa baraza jengine jipya la kutunga katiba mpya ya Misri haukubaliki. Awamu ya pili ya zoezi la kura ya maoni ya katiba mpya ya Misri itafanyika siku ya Jumamosi katika mikoa mingine 17, na matokeo rasmi ya kura hiyo yatatangazwa baada ya awamu hiyo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO