Thursday, December 20, 2012

KUNDI LA JIHADUL ISLAMIYYA LASISITIZAZ HAKI ZA WAKIMBIZI WA PALESTINA

Mwakilishi wa harakati ya Jihadul Islami ya Palestina nchini Lebanon amesisitiza kwa mara nyengine tena juu ya haki ya wakimbizi wa Kipalestina kurejea katika ardh zao za asili. Abu Imad Arrifai, ametoa sisitizo hilo katika mazungumzo na wawakilishi wa makundi na harakati nyengine za muqawama za Palestina na kutahadharisha juu ya njama mbalimbali zinazofanywa na maadui dhidi ya taifa la Palestina. Kiongozi huyo wa Jihadul Islami ameongeza kuwa ardhi ya Palestina ni milki ya wananchi wa Palestina na kwa hivyo lazima wavamizi waondoke katika ardhi hiyo. Zaidi ya wakimbizi laki nne wa Kipalestina wanaishi nchini Lebanon ambao ni sehemu ya Wapalestina zaidi milioni tano wanaoishi kama wakimbizi katika nchi na maeneo mbalimbali duniani baada ya kufukuzwa katika ardhi zao za asili na utawala haramu wa kizayuni wa Israel

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO