MAHMOUD ABBAS APOKEWA KWA SHANGWE
Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmpud Abbas amerudi nyumbani na kukaribishwa kwa shangwe baada ya kushinda idhinisho la uhuru wa Palestina katika Umoja wa Mataifa. Takribani watu 5,000 wamemiminika leo nje ya makao makuu ya serikali ya Abbas katika Ukingo wa Magharibi. Wengi wamebeba bendera za Palestina. Abbas ameuambia umati kwamba sasa wana taifa na ulimwengu umelikubali taifa la Palestina. Uamuzi wa Umoja wa Mataifa wa kuitambua Palestina kama dola mwangalizi isiyo mwanachama wake haubadilishi hali halisi ya mambo. Wapalestina wanaamini kwamba kutambuliwa huko kutaimarisha juhudi za mazungumzo ya amani katika siku za usoni. Kama hatua ya kupinga uamuzi wa Umoja wa Mataifa, Israel leo imetangaza kuwa itazuia zaidi ya dola milioni 100 inazokusanya kama kodi kutoka kwa Wapalestina.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO