Sunday, December 02, 2012

WACHEZAJI SOKA ULAYA HAWATAKI MECHI ISRAEL


Wachezaji soka kutoka ligi kubwa barani Ulaya wamekosoa vikali uamuzi wa Shirikisho la Soka Bara Ulaya UEFA kuandaa kombe la ubingwa wa chini ya umri wa miaka 19 huko Israel mwakani.Katika taarifa, wachezaji hao wamelaani hujuma ya hivi karibuni ya utawala haramu wa Israel dhidi ya Ukanda wa Ghaza na wametangaza mfungamano wao na watu wa Ghaza ambao wanaishi katika mzingiro ambapo wamenyimwa haki za kimsingi za binaadamu na uhuru. Eden Hazard, Yohan Cabaye na Abou Diaby ni kati ya wachezaji kadhaa wa Ligi ya Primia ya England nchini Uingereza ambao wanaunga mkono kampeni hiyo na pia wamekosoa vikali hatua ya Israel kuendelea kuwashikilia bila kuwafunguliwa mashtaka wachezaji soka wawili Wapalestina. Mapema mwaka huu nyota wa zamani wa Manchester United Eric Cantona aliwaandikia barua waandalizi wa mchuano huo na kusema kila siku Israel inatekeleza sera za ubaguzi, ukiukwaji wa haki za binaadamu na ukiukwaji wa sheria za kimataifa. Amesema kama ambavyo nchi za Ulaya zinashinikiza mataifa mengine yaheshimu haki za binaadamu, zinapaswa pia kuishinikiza Israel iheshimu haki za Wapalestina. Mkuu wa Shirikisho la Soka Palestina Jibril Rajoub pia amemundikia barua mkuu wa UEFA Michel Platini akitaka mechi hizo zisichezwa Israel lakini Platini amekataa kutekeleza ombi hilo.


No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO