Sunday, December 16, 2012

MAREKANI KUSAMBARATIKA MUDA SI MREFU : GORBACHEV

Mikhail Gorbachev kiongozi wa zamani wa Umoja wa Kisovieti ametahadharisha kuwa, endapo Marekani itaendelea na siasa zake za kupenda kujitanua, itakumbwa na hatima ya kusambaratika kama iliyoupata Umoja wa Kisovieti. Kiongozi huyo wa mwisho wa Umoja wa Kisovieti amesema hayo katika mkutano kuhusu mustakabali wa Mashariki ya Kati na Bahari Nyeusi huko Istanbul Uturuki na kubainisha kwamba, kugawanyika na kusambaratika Umoja wa Kisovieti kulikuwa ni matokeo ya makosa yake na kwamba, kama Marekani itaendelea na makosa yake haya ya kung'ang'ania kushikamana na siasa zake za kujitanua itakumbwa na hatima kama hiyo. Gorbachev amesema kuwa, kukaliwa kwa mabavu Afghanistan na Umoja wa Kisovieti katika kipindi cha Vita Baridi yalikuwa moja ya makosa yasiyosameheka na kuongeza kwamba, kwa sasa Marekani iko katika mkondo huo huo wa kutaka kukariri makosa yaliyofanywa na Umoja wa Kisovieti. Umoja wa Kisovieti ulisambaratika rasmi 1991 na nchi 15 kujitangazia mamlaka ya kujitawala na kwa muktadha huo, Vita Baridi vikawa vimefikia tamati.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO