Sunday, December 02, 2012

MISIKITI MINNE YABOMOLEWA BAHRAIN

Wanajeshi wa Bahrain wamebomoa Misikiti mingine minne katika eneo la Karzakan ikiwa ni katika njama zao za kuwakandamiza waandamanaji wa nchi hiyo wanaotaka kuuangusha utawala wa kifalme wa Aal Khalifa nchini humo. Hatua ya wanajeshi kubomoa Misikiti hiyo imechukuliwa baada ya kupata kibali kutoka Wizara ya Sheria na hali kadhalika Wizara inayohusiana na masuala ya Kiislamu na Wakfu za nchini humo.


 Taarifa zinasema kuwa, wanajeshi hao licha ya kuharibu Misikiti hiyo, mabuldoza yalikanyagakanyaga Qurani Tukufu zilizokuwemo ndani ya Misikiti hiyo, kitendo ambacho kilizidi kuamsha hasira na chuki za wananchi wa Bahrain dhidi ya utawala wa Mfalme Hamad bin Issa Aal Khalifa. Wizara hizo zimedai kuwa, Misikiti hiyo ilijengwa bila ya kibali, jambo ambalo wananchi wa Bahrain wanasema ni uwongo, kwani Misikiti hiyo kwa miaka mingi ilikuwa ikisaliwa na Waislamu wa Madhehebu ya Kishia wanaokandamizwa nchini humo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO