Sunday, December 02, 2012

PALESTINA NI KADHIA YA UMMA WA KIISLAM NA WAARABU

Waziri Mkuu wa serikali halali ya Palestina amesema kuwa kadhia ya Palestina ni suala muhimu na kuu linalouhusu umma mzima wa Kiislamu na Kiarabu. Akiukaribisha ujumbe wa Yemen katika mji wa Ghaza hii leo Ismail Hania ameeleza kuwa suala la Quds ni jambo linalowahusu Waislamu wote na kwamba Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza wanatetea urithi wa umma wa Kiislamu na Kiarabu. Waziri Mkuu wa serikali halali ya Palestina amesisitiza kwamba ushindi wa Wapalestina katika vita vya siku nane huko Ghaza ni ushindi kwa umma wa Kiislamu na Kiarabu. Hania ameongeza kuwa Ghaza na Palestina haziko pekee katika kukabiliana na adui Mzayuni, jinai zake na mzingiro wa kiuchumi uliowekwa dhidi ya raia wa eneo hilo, bali umma wa Kiarabu na Kiislamu pia ni waungaji mkono wa wananchi wa Palestina.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO