Serikali ya Afrika Kusini imesema kwamba rais wa zamani Nelson Mandela leo amefanyiwa upasuaji wa kuondoa mawe ya nyongo na kwamba anaendelea kupata nafuu. Mandela mwenye umri wa miaka 94, alilazwa hospitalini wiki iliyopita na kufanyiwa vipimo kadhaa vya matibabu. Serikali awali ilisema kwamba mshindi huyo wa tuzo ya amani ya Nobel alikuwa anaugua maambukizi ya mapafu, baada ya kulazwa hospitalini mapema mwaka wa 2011 kutokana na matatizo ya kupumua. Hapo kesho chama cha Mandela cha African National Congress ANC kitaandaa mkutano ambapo kitawachagua viongozi wapya na kuamua kuhusu mwelekeo wa sera zake.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO