Sunday, December 16, 2012

NATO WAKATAA KUINGIA KIJESHI SYRIA


 Mkuu wa Kamisheni ya Kijeshi ya Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi NATO amesema kuwa, uingiliaji wowote wa kijeshi nchini Syria ni suala lisilowezekana. 

Hayo yamesemwa jana na Jenerali Knud Bartels Mkuu wa Kamisheni ya Kijeshi ya NATO katika kikao cha maafisa wa ngazi za juu wa jeshi la Urusi mjini Moscow. Kuhusiana na baadhi ya ripoti zilizoenezwa juu ya uwezNekano wa Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi NATO kutekeleza mashambulizi ya kijeshi nchini Syria, Bartels amesema kuwa, NATO haina mpango wowote wa kutekeleza oparesheni za kijeshi nchini humo. Aidha mbali na kiongozi huyo kukanusha suala hilo, pia amedai kuwa, NATO haina mpango wa kuyasaidia makundi ya kigaidi yanayotekeleza mauaji nchini humo. Hii ni katika hali ambayo baadhi ya nchi za Magharibi hususan Marekani, Uingereza na Ufaransa kwa kushirikiana na nchi za Uturuki, Qatar na Saudi Arabia zimekuwa zikitoa misaada ya kilojestiki na kifedha dhidi ya makundi hayo ya kigaidi kwa lengo la kuuangusha utawala wa Rais Bashar Al-Asad wa Syria.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO