Utawala haramu wa Kizayuni, umekiri kuongezeka uwezo wa muqawama wa Kiislamu wa Palestina Hamas. Jana redio ya Kizayuni ya Shlomo iliwanukuu maafisa wa jeshi la utawala huo wakisema kwamba, Harakati ya Muqawama wa Palestina Hamas inamiliki uwezo mkubwa kuliko wakati mwingine wowote na kwamba suala hilo linashuhudiwa wazi katika sherehe za maadhimisho ya kuasisiwa harakati hiyo, ambazo zimekuwa zikifanyika katika maeneo tofauti huko katika ardhi za Palestina. viongozi hao wa kijeshi wa Kizayuni wameonya juu ya kuongezeka uwezo wa harakati hiyo na kusisitiza kwamba, hali ya usalama katika maeneo tofauti ya Palestina hususan katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, imeanza kurejea suala ambalo limeongeza wasi wasi wa utawala huo bandia. Itakumbukwa kuwa, katika mashambulizi ya Wazayuni hivi karibuni dhidi ya Ukanda wa Gaza, Israel ilishindwa vibaya na muqawama na kulazimika kukubaliana na Hamas kusitisha vita.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO