Saturday, December 22, 2012

ASKARI WA KIKOSI CHA KULINDA AMANI SUDAN AUA WENZAKE

Msemaji wa Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa huko Darfur nchini Sudan UNAMID amesema kuwa, askari mmoja wa kikosi hicho amewauwa wenzake watatu kwa kuwafyatulia risasi na kisha kujiua mwenyewe huko Darfur. Aisha al Basri alikataa kutoa taarifa za nchi wanakotoka askari hao waliouawa. Amesema, shambulio hilo limetokea katika kambi  ya UNAMID iliyoko katika eneo la Mukjar magharibi mwa Darfur, na kwamba uchunguzi umeshaanza kujua chanzo cha vifo hivyo. Hii ni katika hali ambayo, siku chache zilizopita Ban Ki moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Bi. Nkosazana Dlamini Zuma Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika walitoa taarifa ya kumteua Muhammad bin Chembers Mwenyekiti wa zamani wa Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Magharibi mwa Afrika ECOWAS raia wa Ghana kuwa Mkuu wa Vikosi vya UNAMID. Chembers ataongoza wanajeshi na maafisa wa polisi zaidi ya elfu ishirini na moja katika jimbo la Darfur. Chambers anachukua nafasi ya Ibrahim Gambari raia wa Nigeria ambaye kipindi chake kinamalizika mwaka huu

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO