Friday, December 14, 2012

NJIA KUMI ZA KUHIFADHI QUR' AN. Part 3


2. HATUA YA PILI UMUHIMU WA KUPOKEA NA KUISIKIA KUTOKA MDOMONI
 Qur-aan Tukufu siyo kama vitabu vingine ambayo inatosha kutazama na kuisoma ambayo mtu anajitegemea nafsi yake kwani huwezi kutazama katika Mus-haf na kutamka lafdhi bali inahitajika katika kuisoma Qur-aan na Kuihifadhi kuipokea na kusomeshwa kutoka kwenye mdomo wa wasomi na wajuzi wa Tajwiyd (elimu iliyopokelewa kutoka kwa Mtume [Swalla Allaahu ‘alayhi wasallam]). 
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala): “Na hakika wewe unafundishwa Qur-aan inayotokana kwa (Mwenyezi Mungu) Mwenye hikima, Mjuzi.” An-Naml: 6
 
Alikuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wasallam) akiwatamkisha Maswahaba zake Qur-aan, Imekuja kutoka kwa ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuwa aliwaambia Maswahaba wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wasallam): “Hakika Mtume wa Allaah anawaamrisha, asome kila mmoja wenu kama alivyofundishwa.” 
Na hakuna yeyote aliyehifadhi Qur-aan kwa jitihada zake binafsi bila ya kuchukua kwa Mashaykh ila atakuwa mwenye kukosea katika kisomo chake, tuchukulie Mus-haf ya Rasm (mchoro/ maandishi) ya ‘Uthmaaniy haisomwi kama ilivyoandikwa baadhi ya herufi mfano neno “Asw-Swallawaata, Az-Zakawaata” hiyo waaw haitamkwi bali inasomwa “Asw-Swallaata, Az-Zakaata” hivyo katika masharti ya kisomo Sahihi ni kuisoma kutoka kwa Shaykh au Mwalimu. 


 3. HATUA YA TATU UMUHIMU WA KUIHIFADHI KWA TAJWIYD


 Anasema Ibn Jawziy: “Na kuisoma kwa Tajwiyd ni jambo la lazima, na asiyeisoma Qur-aan kwa Tajwiyd anapata madhambi.” Na maana ya Tajwiyd ni kuchunga hukmu za kisomo zilizopo katika vitabu vya Tajwiyd katika Idghaam, Idhwhaar, Ikhfaa, Ghunah, Madda na kuchunga sehemu za kutoa herufi na nyinginezo. Kwani Qur-aan Kariym inatofautiana na vitabu vingine, ni Maneno ya Allaah na kwa mpangilio huu amepokea Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wasallam) kutoka kwa Jibriyl kutoka kwa Mola Mtukufu na hivyo ndivyo ilivyotufikia. Imepokewa kutoka kwa Ibn Mas’uud alikuwa mtu anamsomea neno lake Mwenyezi Mungu:     At-Tawba: 60 “إِنَّمَا الصَّدَقَاتُ لِلْفُقَرَاء Alisoma neno “Al-Fuqaraa لِلْفُقَرَاء” bila ya kuvuta Madda, akasema Ibn Mas’uud sivyo hivyo alivyonifundisha Mtume wa Allaah akamwelekeza avute Madda baada ya herufi ya raa.
 
Haina maana uzame katika elimu ya Tajwiyd kwa undani kupita kiasi, muhimu uweze kuisoma Qur-aan kwa hukmu na kujua Tafsiyr yake ili uweze kuifanyia kazi. 
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala): “Wale katika (Ahlul Kitaab) tuliowapa Kitabu (Taurati, Injili, Zaburi…) wakakisoma kama ipasavyo kukisoma (bila ya kupotea Tafsiri yake wala kutoa hili na kutia lile), hao huiamini hii Qur-aan wakasilimu). Na wanaokikanusha (hicho Kitabu chao wakapinduapindua tafsiri yake na wakaongeza na wakapunguza), basi hao ndio wenye hasara.” Al-Baqarah: 121
 itaendelea Ijumaa ijayo insh-Allah...............

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO