Saturday, December 22, 2012

NRA MATATANI NCHINI MAREKANI


Hisia mbali mbali zinaendelea kutolewa nchini Marekani baada ya Mkuu wa Jumuiya kubwa inayotetea umiliki wa bunduki nchini humo NRA, Wayne LaPierre kusema polisi wenye silaha lazima wawekwe katika shule zote nchini Marekani ili kuwalinda watoto dhidi ya wahalifu.
Seneta aliyeteuliwa wa chama cha Demokrats, Chris Murphy amesema hajawahi kusikia jambo la kuchukiza maishani mwake kama hilo, naye kamishna wa polisi wa jimbo la new york, Ray Kelly amesema amevunjika moyo na tamko hilo.
Baadhi ya raia nchini Marekani wanaunga mkono hatua hiyo huku wengine wakipinga na kusema kuwa ni hatua itakayowasumbua watoto akili kuona maaskari na bunduki shuleni kila wakati. Tamko la NRA linakuja wiki moja baada ya mauaji ya watoto 20 na watu wazima  6 yaliofanywa na mshambuliaji katika shule  ya  Sandy Hook mjini Newtown Marekani.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO