Saturday, December 22, 2012

MAUAJI YA KUTISHA YATOKEA NCHINI KENYA


Watu wasiopungua 41 wameuliwa kwa umati katika shambulizi la kushitukiza la alfajiri kwenye kijiji kimoja cha ndani huko Tana Delta nchini Kenya.
Watu wasiojulikana wamekivamia kijiji cha Kipao huko Tana River Delta alifajiri ya kuamkia leo na kuua kwa umati makumi ya watu na kujeruhi makumi ya wengine. Habari kutoka nchini Kenya zinasema kuwa mauaji hayo yalifanyika saa tisa usiku kuamkia leo na mbali na kuuawa watu 41 wakiwemo wanawake na watoto wadogo, yamepelekea kujeruhiwa pia watu wengine 35. Watu waliojeruhiwa waliwahishwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Malindi ambako wanaendelea kupata matibabu.
Wavamiaji hao waliwacherenga kwa mapanga na kuwapiga risasi wanavijiji hao wakati wakiwa wamelala na kupelekea baadhi yao kukimbilia msituni usiku wa manane licha ya kuweko wanyama wakali. Mwezi Agosti na Septemba mwaka huu pia zaidi ya watu 100 waliuliwa katika machafuko kama hayo kwenye eneo hilo na kuilazimisha serikali kutuma mamia ya askari wake kwenye eneo hilo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO