Friday, December 14, 2012

OPEC YASEMA VIKWAZO VYA MAFUTA IRAN SIFURI

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi duniani OPEC amesema kuwa, takwimu zinaonyesha kuwa vikwazo vya mafuta vya upande mmoja vya Marekani na nchi za Magharibi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, havina tathira yoyote.
 
Abdullah Al- Badri aliyasema hayo jana na kuongeza kuwa, takwimu zinaonyesha kwamba, Iran kwa kila siku inaendelea kuzalisha mapipa milioni 3.7 ya mafuta. Mwezi uliopita Wakala wa Kimataifa wa Nishati na ambayo ni taasisi ya utafiti yenye makao yake mjini Paris Ufaransa, ulidai kuwa, mwezi Novemba mwaka huu uzalishaji wa mafuta nchini Iran ulipungua na kufikia kiwango cha mapipa milioni 2.7 kwa siku, suala ambalo linapingana na takwimu za jumuiya ya Opec.
 

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO