Saturday, December 22, 2012
SUDAN YA KUSINI YAKIRI KUITUNGUA NDEGE YA UN
Msemaji wa Jeshi la Sudan Kusini amekiri kwamba jeshi la nchi hiyo limeitungua helkopta ya Umoja wa Mataifa katika eneo la Likuangole, jimbo la Jonglei huko Sudan Kusini. Philip Aguer ameongeza kuwa, jeshi la nchi hiyo lilidhani kwamba helkopta ya Umoja wa Mataifa ni ndege ya adui na hivyo kuitungua. Kwenye tukio hilo, wafanyakazi wote wanne raia wa Russia waliokuwa ndani ya helkopta hiyo walipoteza maisha. Amesema kuwa, kulikuwa hakuna mawasiliano yoyote kwamba helkopta ya Umoja wa Mataifa itapita katika eneo hilo. Wakati huohuo, Ban Ki moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani vikali kitendo cha kutunguliwa helkopta hiyo ya kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa huko Sudan Kusini UNMISS na kuitaka serikali ya Juba kufanya uchunguzi wa kina na wote waliohusika na shambulio hilo wafunguliwe mashtaka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO