Saturday, December 22, 2012

HIZBULLAH WATAKA MAZUNGUMZO YA KITAIFA

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah amesema kuwa kuna ulazima wa kuanzishwa mazungumzo ya kitaifa nchini humo. Akizungumza na Mustafa Hamdan Mkuu wa Harakati ya Mustaqil Nasir ya Lebanon, Sheikh Naim Qasim ameongeza kuwa, kuanzishwa mazungumzo hayo na kuwekwa pembeni hitilafu zilizopo baina ya makundi ya kisiasa ya nchi hiyo, kunaweza kutoa huduma kubwa kwa wananchi wa Lebanon. Akielezea hatua ya mrengo wa March 14 wa kususia vikao vya bunge la Lebanon, Sheikh Naim Qassim ameongeza kuwa, lengo la kususiwa vikao hivyo ni kuukwamisha mwenendo wa kupitishwa sheria mpya ya uchaguzi, na hali kadhalika mrengo huo unataka utekelezwaji wa mpango huo baada ya kumalizika mgogoro wa Syria. Sheikh Qassim amesisitiza kuwa, mrengo wa March 14 unapaswa kuelewa kwamba wananchi na serikali ya Syria wataibuka na ushindi kwenye mapambano dhidi ya maadui. Sa'ad Hariri Waziri Mkuu wa zamani wa Lebanon ambaye ni kinara wa mrengohuo unaoungwa mkono na Wamagharibi katika miezi ya hivi karibuni amekuwa akisusia vikao vya mazungumzo ya umoja wa kitaifa baada ya kuondolewa madarakani. Hata hivyo, mrengo huo unataka Hizbullah ipokonywe silaha, katika hali ambayo silaha za Hizbullah zinatumika kwa shabaha ya kukabiliana na mashambulizi na vitisho vya majeshi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO