UTURUKI YAKARIPISHA MITAMBO YA ULINZI TOKA NATO
Uturuki imekaribisha hatua ya Muungano wa Kijeshi wa Nato ya kukubali kuweka makombora ya Patriot kwenye mpaka wa nchi hiyo na Syria. Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki imedai kuwa hatua zilizochukuliwa na Ankara kivyovyote vile hazina lengo la kutekeleza hujuma yoyote ya kijeshi na kwamba lengo la kuweka ngao hiyo ya makombora ni kwa ajili ya kulinda ardhi ya Uturuki. Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki imeongeza kudai kuwa makombora ya anga na ardhini ya Patriot hayatatumika kwa ajili ya kuasisi eneo lisiloruhusu kuruka ndege huko Syria. Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Muungano wa Nato waliafiki ombi la serikali ya Ankara la kuweka aina hiyo ya makombora katika mpaka wake na Syria katika kikao chao cha jana huko Brussels Ubelgiji. Ngao hiyo ya makombora inatazamiwa kuwekwa huko kusini mwa Uturuki katika kipindi cha wiki kadhaa zijazo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO