Sunday, December 23, 2012

WAASI YA SYRIA WATUMIA SILAHA ZA KEMIKALI

Waasi wanaopigana dhidi ya serikali ya Syria wametumia silaha za kemikali dhidi ya jeshi la nchi hiyo huko Daraya karibu na mji mkuu Damascus. Hayo yamesemwa na jeshi la Syria. Kamanda wa gadi ya ulinzi ya Rais Bashar al Assad wa Syria amesema kuwa wanajeshi wa nchi hiyo wasiopungua saba waliuliwa jana baada ya kushambuliwa kwa silaha za kemikali zinazotoa gesi ya njano yenye sumu.

 Amesema wanajeshi hao waliripotiwa kufariki dunia saa moja baada ya kuvuta gesi hiyo yenye sumu. Makundi ya kigaidi nchini Syria yanayoungwa mkono na nchi za kigeni hivi karibuni yalitishia  mara kadhaa kwamba yatatumia silaha za kemikali dhidi ya jeshi la Syria na raia wanaoiunga mkono serikali ya nchi hiyo. Magaidi hao aidha wametishia kuyachafua maji ya kunywa ya Syria katika njama yao ya kutaka kuwauwa wananchi wa nchi hiyo. Kabla ya hapo pia waasi wa Syria walitoa mkanda wa video unaoonyesha namna sungura wa maabara walivyokuwa akikata roho baada ya kuvuta gesi hiyo yenye sumu.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO