Friday, December 07, 2012

WATAALAMU WA SAUDI ARABIA WAUNDA ''SCREW'' YA KUFUNGIA MIFUPA


 Ofisi ya hakimiliki ya ulaya (EPO)  imewapa hakimiliki wataalamu wawili wa Saudi Arabia kutokana na uvumbuzi wao wa msumari 'screw' ambao wameutengeneza wenye madini ya asili,  na wao wameipa jina la ‘’Date stones’’.

Muundo wa screw hiyo unafanana na muundo wa mifupa kwa sababu ina wanga(carbohydrates), protini(proteins), nyuzinyuzi(fiber), chumvicumvi (minerals).
Screw hiyo itakuwa ikitumika katika upasuaji wa kufunga makundi mbalimbali ya  mfupa hasa ile iliyovunjika , ambapo itakaa katika mifupa iliyounganishwa na huanza kuoza kwa kawaida katika mwili baada ya kipindi cha siku 30-45, kuanzia tarehe ya upasuaji. Mtengano au kuoza kikamilifu inahitaji muda wa miezi sita hadi tisa.

"Hii screw mpya ni maendeleo makubwa katika sayansi ya utabibu. Utofauti wa screw hii na zingine ni  kutokana na kwamba screws nyingine za  chuma zimetengenezwa na chrome au metali nyingine kwa njia nyingi tofauti. Ubora wa screw hii ni kwamba inatengana na mwili bila matatizo yoyote na bila kuleta athari yoyote mbaya, " walisema katika  taarifa yao ya pamoja wavumbuzi hao wawili, Mohammed Assa'edi na Nagwan Abu Khair.

Screw  hii haihitaji upasuaji  wa kuiondoa  katika mwili baada ya mfupa iliyoungwa kupona kama ilivyozoeleka sasa kwenda kufanyiwa upasuaji mwingine wa kuondoa vyuma . Pia ni rahisi kutumia na itakuwa ni bei nafuu. Khaled Saleh, mkurugenzi wa Miliki ya Teknolojia katika chuo kikuu cha mfalme Saud , alisema mpango huo tayari umeshapokea hakimiliki kutoka kwa EPO. Timu ya kisayansi katika chuo kikuu  hicho zitaanza majaribio ya kliniki kwa kuitumia screw hiyo, katika maandalizi kwa ajili ya matumizi yake, ndani ya nchi na kimataifa.

Taasisi ya EPO ina wajumbe 146 kimataifa. Nchi zenye uvumbuzi muhimu wa kisayansi na kibiashara huchaguliwa kwa kusudi hili, ikishirikiana na Ofisi ya hakimiliki ya Ulaya, Marekani, Canada, Uingereza, Ujerumani na Ufaransa. 

SOURCE:  http://www.arabnews.com/two-saudis-invent-bone-screw-date-stones


No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO