wanapaswa kubadili misimamo yao mkabala na Iran, ili kufanikisha mazungumzo kati ya Jamhuri ya Kiislamu na kundi la 5+1. Mehdi Senai aidha ameongeza kwamba, kwa kawaida nchi za Magharibi hutangaza kuchukua misimamo chanya lakini hutekeleza siasa zilizo kinyume chake na kuiwekea vikwazo vipya Iran. Aidha amesema, misimamo hiyo inayokinzana huzuia kupatikana mafanikio kwenye mazungumzo hayo. Iran imefanya duru kadhaa za mazungumzo na kundi la 5+1 linalozijumuisha nchi za Uingereza, China, Ufaransa, Russia, Marekani na Ujerumani lengo kuu likiwa ni kujadili mipango ya nyuklia ya Iran, lakini bado hakujapatikana mafanikio yoyote ya maana kutokana na ukwamishaji wa baadhi ya pande za Magharibi.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO