Wednesday, January 16, 2013

ALSHABAB WATISHIA KUMUUA MATEKA WA KIFARANSA


Kundi la wanamgambo wa al Shabab nchini Somalia limetishia kumuua mateka linayemshikilia wa Ufaransa. Kundi hilo limechukua uamuzi huo wa kumuua Denis Allex, ajenti wa shirika la ujasusi la Ufaransa, baada ya makomandoo wa Kifaransa kushindwa kwenye operesheni ya kijeshi ya kumuokoa mateka huyo nchini Somalia. Taarifa kutoka Mogadishu zinasema kuwa, wanajeshi wawili wa Kifaransa wameuawa katika operesheni hiyo.
Ujumbe uliotolewa na kundi la wanamgambo wa al Shabab kwa serikali ya Ufaransa unaeleza kuwa, katika siku zijazo wananchi wa Ufaransa wataomboleza msiba wa jasusi huyo. Inafaa kuashiria hapa kuwa, hivi karibuni Rais Francois Hollande wa Ufaransa alikubali kubeba lawama za kushindwa makomandoo wa nchi hiyo katika operesheni ya kumuokoa mateka huyo anayeshikiliwa na kundi la al Shabab tokea mwaka 2009.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO