Wednesday, January 16, 2013

NATO YAHOFIA UWEZO WA HIZBUL LAH


Jumuiya ya Kijeshi ya Nchi za Magharibi NATO imeingiwa na wasiwasi mkubwa kutokana na kuongezeka nguvu na uwezo wa kijeshi wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon.
Taarifa ya NATO imedai kuwa, Hizbullah ya Lebanon ina wapiganaji wasiopungua elfu sitini na tano, na kwamba ni vigumu kukabiliana na kikosi kama hicho. Kabla ya hapo, mwakilishi wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika Umoja wa Mataifa alikiri kwamba nguvu za kijeshi za Hizbullah zimeongeza sana na kusisitiza kuwa, harakati hiyo imeweza kuongeza nguvu zake za kisiasa na kijeshi hali ambayo ni jinamizi kubwa kwa viongozi wa utawala wa Israel.
Utawala wa Kizayuni wa Israel mwaka 2006 ulianzisha mashambuzi ya siku 33 dhidi ya Hizbullah kwenye ardhi ya Lebanon na hatimaye majeshi ya utawala huo ghasibu yalilazimika kuondoka kwa madhila kusini mwa nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO