Wednesday, January 16, 2013

BAN AITAKA ISRAEL IACHE UJENZI WAKE WA VITONGOJI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameutaka utawala wa Kizayuni wa Israel ufute mpango wake wa ujenzi wa vitongoji vipya vya walowezi wa Kizayuni katika ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Ban Ki-Moon amewataka viongozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wafute mpango wao huo. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa, ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi huko katika Ukongo wa Magharibi wa Mto Jordan ni haramu na unaokinzana na sheria za kimataifa. Habari kutoka Palestina zinasema kuwa, viongozi wa Israel wameongeza kasi ya ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi kama moja ya njia za kufidia kushindwa kwake katika vita vya siku nane mbele ya wana muqawama shupavu wa Kipalestina. Hivi karibu viongozi wa Israel walipasisha mpango wa ujenzi wa nyumba mpya elfu sita katika eneo la Quds Mashariki na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Utawala wa Kizayuni wa Israel umeendelea kupuuza kabisa misingi ya sheria za kimataifa hususan azimio la mwezi Desemba mwaka jana la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na hivi sasa unaendelea na hatua zake za kubadilisha utambulisho wa maeneo ya Wapalestina huko Baytul Muqaddas katika fremu ya stratejia yake ya kuyayahudisha maeneo ya Wapalestina.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO