Sunday, January 13, 2013

HALI YA HEWA BEIJING YACHAFUKA

Beijing



Kuchafuka kwa hali ya hewa katika mji mkuu wa uchina, Beijing, kumefikia kiwango kibaya kabisa kuwahi kutokea kwa miaka kadha. Mwandishi wa BBC mjini Beijing anasema kwa siku kadha sasa kumekuwa na ukungu mzito, na hewa ina ladha ya moshi wa makaa na magari.Vipimo rasmi vya uharibifu wa hewa vimepindukia kiwango ambapo watoto wote pamoja na wazee huambiwa wasitoke nje. Hata ndani ya nyumba kumetanda. Moshi kama huo huleta shida za kupumua na kuzidisha idadi ya watu wanaokufa kwa sababu ya saratani ya mapafu na ugonjwa wa moyo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO