Monday, January 14, 2013

ALGERIA, TUNISIA NA LIBYA WASAINI MAKUBALIANO.


Algeria, Tunisia na Libya zimesaini makubaliano ya kiusalama kati yao. Taarifa ya pamoja iliyotolewa na nchi hizo tatu inaeleza kuwa, Mawaziri wa nchi tatu za Kiafrika yaani Algeria, Tunisia na Libya wamesaini makubaliano ya kiusalama ili kuhakikisha kuwa amani inakuwepo kwenye mipaka ya nchi hizo na kupambana na magendo ya madawa ya kulevya na jinai zilizoratibiwa kati ya nchi hizo.
Kwa mujibu wa makubaliano hayo ya pande tatu, Algeria, Tunisia na Libya zitazidisha doria za upekuzi za vikosi na idara za usalama kwenye mipaka ya nchi hizo. Waziri Mkuu wa Libya amesema kuwa yeye na wenzake wa Algeria na Tunisia wameamua kuchukua hatua hiyo kwa kuzingatia mgogoro uliojitokeza huko Mali.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO