Wednesday, January 16, 2013

HIZBUL LAH YALAANI MAUAJI YA PAKISTAN


Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon Hizbullah imelaani vikali mauaji yanayofanywa na makundi kigaidi ya kufurutu ada nchini Pakistan. Hizbullah ilitoa taarifa hiyo jana na kusema kuwa, mashambulizi dhidi ya Waislamu wasio na hatia wa madhehebu ya Kishia nchini Pakistan, yanafanana kabisa na mashambulizi ya miripuko ya mabomu yanayofanywa na makundi ya kigaidi nchini Iraq, Syria na Afghanistan na kwamba, jinai hizo zinafanyika chini ya mpango wa Marekani na utawala haramu wa Kizayuni kwa lengo la kuzusha fitna kati ya Waislamu nchini humo. Aidha Harakati hiyo ya Hizbullah imetoa mkono wa pole kwa familia za wahanga wa mauaji hayo na kusema kuwa, njama hizo zinafanyika chini ya fremu ya kuharibu sura halisi ya Uislamu na kwamba, njama hizo zitagonga mwamba tu.
Wakati huo huo, srikali ya Lebanon imekosoa vikali hatua ya serikali ya Ufaransa ya kushindwa kumuachilia huru, mwanaharakati wa nchi hiyo George Abdullah aliyemaliza kuhudumu kifungo chake cha miaka 28 nchini Ufaransa na kusema kuwa, hatua hiyo inakinzana na sheria za kimataifa.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO