Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa ustawi wa kasi wa Iran katika uzalishaji elimu ni jambo ambalo linapaswa kupongezwa.
Akizungumza Jumanne katika Tamasha la 18 la Razi la Utafiti wa Sayansi za Tiba, Rais Ahmadinejad amesema kwamba, Iran ina uwezo wa kuwa kati ya nchi zinazoongoza katika ustawi wa elimu ya juu. Ameongeza kuwa mafanikio ya kielimu yanayopatikana nchini ni kwa ajili ya kuhudumia jamii ya wanaadamu wote. Rais Ahmadinejad amesema katika kipindi cha mwezi mmoja ujao, Iran itazindua aina 30 za madawa mapya.
Rais Ahmadinejad Iran ina uwezo wa kuongoza katika uga wa tiba kwani historia imejaa mifano ya namna Wairani waliweza kuleta fakhari kubwa katika uga wa tiba na uhandisi. Rais wa Iran pia ameongeza kuwa madola ya kibeberi duniani yanatengeneza mabomu ya vijidudu kwa lengo la kuwaangamiza wanaadamu na kueneza magonjwa ili kufaidika katika biashara ya madawa katika hali ambayo taaluma ya tiba Iran inatazamwa kama taaluma takatifu isiyopaswa kufunganisha na masuala ya faida za kifedha.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO