Wednesday, January 16, 2013

UFARANSA KUPELEKA WANAJESHI 2500 MALI

Wizara ya Ulinzi nchini Ufaransa imetangaza kuwa, itapeleka hatua kwa hatua askari wake wapatao 2,500 huko nchini Mali. Kwa mujibu wa gazeti la Kifaransa la Le Figaro kutoka kwa mtu wa karibu na Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo, wizara hiyo imesema kuwa, katika kupambana na makundi ya magaidi yanayoyadhibiti maeneo ya kaskazini mwa Mali, Paris, imeazimia kupeleka kwa hatua askari wake 2,500 katika nchi hiyo. Hayo yanajiri katika hali ambayo, mapema leo Rais François Nicolas Holland wa Ufaransa amenukuliwa akisema mjini Abudhabi, Imarati kuwa, hadi sasa nchi yake imekwishatuma nchini Mali askari wapatao 750 na kwamba, idadi ya askari hao inatarajiwa kuongezeka hapo baadaye. Pamoja na Paris kukabiliwa na mgogoro mkubwa wa kiuchumi, imeingia vitani nchini Mali kwa kisingizio cha kupambana na magaidi. Makundi ya waasi ambayo tangu miezi 9 iliyopita yaliyadhibiti maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika, siku ya Alkhamisi iliyopita yalianza kusonga mbele kuelekea mji mkuu wa nchi hiyo, Bamako.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO