Tuesday, January 08, 2013

IRAN YAILAANI HISPASAT KWA KUONDOA TV CHANNEL ZAKE KWENYE SATELITE


Shirika la Kimataifa la Satalaiti (STN) limelaani vikali hatua ya shirika la Kihispania la kutoa huduma za satalaiti la HispaSat kwa kuondosha kanali za televisheni za Irani za Press TV na HispanTV kwenye orodha ya televisheni zinazorushwa hewani kwenye shirika hilo.
Shirika la Kimataifa la Satalaiti (STN) linatarajiwa kufungua mashtaka dhidi ya HispaSat kutokana na maamuzi iliyoyachukua dhidi ya kanali za televisheni za Kiirani. Taarifa ya STN imesisitiza pia juu ya kusimamishwa haraka marufuku dhidi ya kanali za televisheni za Press TV na Hispan TV. Inafaa kuashiria hapa kuwa, tarehe 21 Disemba mwaka 2012, kanali za televisheni za Press TV na Hispan TV zote za Iran ziliondoshwa kwenye orodha ya kanali zitakazorushwa kwenye shirika la HispaSat kwa kisingizio cha vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB.
Nchi za Magharibi na hasa Marekani zinadai kuheshimu uhuru wa kujieleza, lakini zimekuwa mstari wa mbele katika  kuvifunga mdomo vyombo vya habari vya Iran kwa kupiga marufuku kurushwa matangazo ya IRIB kwenye mashirika ya huduma za setelaiti kama vile Eutelsat SA, Intelsat SA na AsiaSat.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO