Tuesday, January 08, 2013

WAISLAM WAANDAMANA KUPINGA NDOA ZA JINSIA MOJA


Waislamu nchini Ufaransa wamepanga kufanya mandamano siku ya Jumapili ijayo kupinga mpango wa kupitishwa sheria rasmi ya ndoa kati ya watu wenye jinsia moja nchini humo.
Serikali ya Kisoshalisti ya Ufaransa imepanga kupitisha sheria hiyo mwezi Juni mwaka huu. Uamuzi huo wa serikali ya Paris unakabiliwa na upinzani mkubwa wa makundi mbalimbali na wafuasi wa dini tofauti nchini humo.
Inakadiriwa kuwa, kuna wafuasi zaidi ya milioni tano wa dini ya Uislamu nchini Ufaransa na dini hiyo inahesabiwa kuwa ya pili kwa kuwa na wafuasi wengi zaidi nchini humo baaada ya dini ya Kikristo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO